Kamwambia wake “Ukipata mwanaume mwengine olewa!”

Swali: Nimemtaliki mke wangu na kumwambia: “Ukimuomba mwanaume kukuoa, olewa” na nikampa karatasi yake (ya Talaka). Je, naweza kumrudi mara ya pili?

Jibu: Talaka ikiwa ni kwa matamshi kama haya, inakuwa imepita mara moja. Akimwambia: “Ukikubaliana na mwanaume mwengine waweza kuolewa”, “mwanaume mwengine akikichumbia, olewa” au mfano wa matamshi kama hayo, au “wewe nimekutaliki”, au “wewe umetalikika” au mfano wa hayo, hii huchukuliwa ni Talaka moja tu. Anaweza kumrudi maadamu bado angali ndani ya eda, kwa kushahidisha mashahidi wawili ya kwamba kamrejea mke wake. Bora zaidi, awashuhudishe mashahidi wawili ambao ni waadilifu, washuhudie ya kuwa kamrudi mke wake maadamu bado angali ndani ya eda, yaani maadamu katwaharika hedhi mara tatu ikiwa ni mwanamke mwenye kupata hedhi. Na ikiwa ni mwanamke ambaye hapati hedhi, eda yake ni miezi mitatu. Akimrudi ndani ya miezi hii mitatu, mwanamke huyo anakuwa ni Halali kuwa mke wake. Ama ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi, eda yake (inaisha) kwa kupata hedhi tatu, ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi. Na ikiwa ni mzee na hapati hedhi, eda yake ni miezi mitatu. Ama ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi, eda yake (inaisha) kwa kupata hedhi tatu, ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi. Na ikiwa ni mzee na hapati hedhi na binti mdogo (ambaye hajaanza kupata hedhi), eda yake ni miezi mitatu. Ikiwa hakumuwahi ndani ya muda wake huyo wa eda, basi mwanamke huyo atakuwa ni ajinabi kwake. Hatokuwa Halali kwake isipokuwa kwa ndoa nyingine mpya kama wanawake wengine ambao anaweza kuwachumbia. Hawi Halali isipokuwa kwa kufunga ndoa mpya na masharti yanayokubalika Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 27/03/2018