Swali: Mimi ni mwanaume ambaye nimeoa na nina matangamano na mke wangu mazuri sana kwa daraja ambayo nilimwambia “uso kukutana na wangu ni Haramu ukinificha kitu kinachohusiana na maisha yetu ya kindoa.” Lakini nimekuja kuona kuwa jambo hili ni khatari, na nataka kuelekezwa katika jambo ambalo litanitoa katika sharti hii. Ipi hukumu ikiwa mke wangu atanificha kitu bila ya mimi kujua?

Jibu: Ikiwa makusudio ni kumkataza asikufiche chochote, inatosha kwako kutoa kafara ya yamini. Na wala sio lazima kwake kukubainishia kila kitu, ikiwa ni mambo yaliyopita. Akubainishie mambo yenye faida. Ama yanayoweza kumdhuru katika mambo ambayo ni maslahi maalumu yanayomuhusu yeye au yakakudhuru wewe, sio lazima kwake kukubainishia. Lakini akubainishie yanayohusiana na maslahi yako na maslahi ya nyumba yako. Na ikiwa unataka kujitoa katika hilo ni juu yako kutoa kafara ya yamini, ni juu yako kutoa kafara ya yamini na inatosha. Kwa kuwa makusudio yako (kusema hivyo) ni kumhimiza kukubainishia kila kitu na wala asikufiche kitu. Ukitoa kafara ya yamini inatosha. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Kama utakula yamini ukaona lingine ni bora kuliko hilo basi lifanye hilo bora na fanya kafara la yamini yako.” Na hii hukumu yake ni kama ya yamini. Ni juu yako kuleta Tawbah juu ya hilo, kwa kuwa kuharamisha ni jambo lisilojuzu. Ni juu yako kutubu kwa Allaah (Ta´ala) na utapotoa kafara ya yamini yako hakuna neno. Muhimu ni wewe utoe kafara kwa yamini yako.

Muulizaji: Hata kama kwa kusema kwake huko amekusudia (mke huyo) kuharamika kwake?

Ibn Baaz: Ikiwa amekusudia kuharamika kwake, huyu ni juu yake kutoa kafara ya Dhwihaar. Ama ikiwa amekusudia kumhimiza (kufanya au kutofanya kitu)… Na hii ndio dhahiri (ya makusudio ya muulizaji). Watu wengi kwa mfano wa hili, wanakuwa wanakusudia kuhimiza ili kumtisha (mke wake). Kwa hali hii atatoa kafara ya yamini. Ama ikiwa ndani ya moyo wake amekusudia kuharamika kikamiifu, hii itakuwa ni Dhwihaar na ni juu yake kutoa kafara ya Dhwihaar. Nayo ni kuacha mtumwa huru, asiyeweza afunge miezi miwili mfululizo na asiyeweza alishe masikini sitini kwa chakula kimechozoelekea mjini; kila masikini atampa 1,5 kg kabla ya kumgusa (kumjamii). Ikiwa alikusudia hili – kuharamika – naye akathibitisha kuwa amemficha kitu, atatoa kafara hii na yatosha. Ama akithibitisha ya kuwa hakumficha kitu, hana juu yake kitu.

Muulizaji: Vipi ikiwa atamficha na asimwambie hilo?

Ibn Baaz: Ikiwa anajua kihakika ya kuwa kamficha kitu, ni juu yake kutoa kafara…

Muulizaji: Lakini nakusudia ikiwa (mke) amemficha kitu wala yeye (mume) hakujua kitu…

Ibn Baaz: Hana juu (mume) kitu. Lakini akimweleza, ni juu yake atoe kafara.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 27/03/2018