Kamwambia mke “Wake Ukibaki nyumbani leo nitakuwa nimekutaliki”


Swali: Kuna siku nilihudhuria nyumbani, nikamkuta mke wangu amefanya kazi ambayo ilinikasirikisha. Nikamwambia “ukikaa nyumbani siku hii ya leo, nitakuwa nimekutaliki”. Akawa ametoka siku hiyo hiyo na kisha akarejea baada ya wiki. Je, ametalikika au hapana? Na je, nina kafara yoyote?

Jibu: Ikiwa makusudio ilikuwa ni kumkataza kubaki siku hiyo na usiku wake tu, hakupiti kitu, kwa kuwa alitoka na hakurudi isipokuwa baada ya wiki. Ama kama makusudio yako ilikuwa ni kutengana nae, makusudio yako sio siku na usiku huu, bali makusudio yako ilikuwa ni kutengana nae na kumtaliki, basi Talaka itakuwa imepita ambayo ulikusudia. Nayo ni Talaka moja, haikupita isipokuwa Talaka moja tu. Ikiwa mwanzoni alikuwa hajamtaliki Talaka mbili, anaweza kumrejea maadamu bado angali ndani ya eda. Hali hii ni kama alikusudia Talaka. Ama ikiwa makusudio yake ilikuwa ni kumkataza siku hiyo tu, kutakuwa hakukupita kitu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 27/03/2018