Kama usengenyi


Swali: Mtu anayesikilizia usengenyi ni kama kusengenya?

Jibu: Ndio. Ikiwa humkatazi na kumshauri unashirikiana naye katika dhambi. Kwa sababu ni dhambi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu basi ayakataze kwa mkono wake, asipoweza afanye hivo kwa mdomo wake, asipoweza afanye kwa kuchukia – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”[1]

[1] Ahmad (3/10) na Muslim (49).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (83) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-15-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/01/2018