“Kama isingelikuwa baba yetu Aadam basi tungelikuwa Peponi”


Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema: “Lau Mtume wetu Aadam asingekula kwenye mti basi tungelikuwa Peponi.” Je, katika maneno haya kuna dhambi?

Jibu: Hili halijuzu. Kusema hivi ni kumsema vibaya Aadam (´alayhis-Salaam). Aadam alitubu kwa Allaah na akamsamehe. Haijuzu kusema hivi.

Ndugu! Iangalie nafsi yako. Hutoingia Peponi bila ya matendo. Huingii Peponi isipokuwa kwa matendo yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13398
  • Imechapishwa: 26/04/2018