Swali: Ni ipi hukumu ya kufunza au kufanya Da´wah kwenye misikiti au vituo vya Ahl-ul-Bid´ah?

Jibu: Kinachotakikana ni kufanya Da´wah kwenye misikiti ya Ahl-us-Sunnah. Lakini mtu akienda kwa watu hao na akawatolea kalima ambapo akabainisha Sunnah na akatahadharisha kutokamana na Bid´ah, basi ni jambo zuri midhali atatumia fursa hiyo kubainisha Sunnah. Ama ikiwa anazungumzia tu kile kitu wanachotaka wao na kutamani, basi asende.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=tWZ2Gf-gaRk&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 10/05/2019