Kalamu iliyoandikwa “Allaah” kuingia nayo chooni


Swali: Baadhi ya kalamu zimeandikwa jina tukufu la Allaah kama vile ´Abdullaah na mfano wake. Ni ipi hukumu ya kuingia nazo chooni?

Jibu: Usiingie nazo kama mfano wa pete. Mtume alikuwa na pete imeandikwa “Muhammad Mtume wa Allaah” na alikuwa akiivua wakati anapoingia chooni. Isipokuwa akichelea kuwa itapotea katika hali hiyo anakuwa ni mwenye kupewa udhuru. Bora ni kutoandika juu ya kalamu chochote kilichoandikwa utajo wa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 05/03/2021