Swali: Inatokea wakati mwingine ninawadhibiti dada zangu kwa ajili ya manufaa yao. Kwa mfano ninamuona mdogo wangu anavuta sigara ninampiga na hilo linakuwa baada ya kumnasihi. Kipigo hichi hakiwi isipokuwa baada ya kukariri kwa kitendo hicho. Kadhalika ni mwenye bidii juu ya vazi la dadangu zangu wadogo na kuwaheshimisha. Lakini hata hivyo ninapofanya hivo mamangu ananikasirikia kwa sababu ya kuwapenda sana. Kutokana na sababu hiyo wanaendelea kuasi na kupuuza ninayosema. Je, ninayoyafanya ni kumuasi mama yangu?

Jibu: Sio kumuasi mama yako. Wewe ni mzuri kwa dada zako, unawalea. Akikuamrisha kutofanya hivo usimtii katika hilo. Kwa sababu anakuamrisha kuacha jambo la wajibu na malezi sahihi. Usimtii katika hili. Mkinaishe na umfanye afahamu kuwa ni kwa ajili ya manufaa yao wenyewe. Hata hivyo usiwapige vibaya. Kusiumize sana. Inatakiwa iwe kipigo kisichoumiza. Isiwe zaidi ya vipigo tano.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 03/06/2018