Kafiri ni lazima abadili jina lake anaposilimu?

Swali: Ni ipi hukumu ya kujiita kwa jina la manaswara? Je, kafiri ni lazima kubadili jina lake anaposilimu?

Jibu: Haijuzu kujifananisha na manaswara katika majina yao, mavazi yao, majina yao na ´ibaadah zao.

“Yule mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao.”

Kama anavyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Usijifananishe na mayahudi na manaswara. Haijuzu kujifananisha na mayahudi na manaswara, katika hayo ni kujiita kwa majina ambayo ni maalum kwao kwa ajili ya kujifananisha nao. Majina ni mengi ambayo ni rahisi. Mtu achague lile ambalo ni zuri. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Jina bora ni ´Abdullaah na ´Abdur-Rahmaan.”

Apewe uabudiwa mtoto kwa Allaah. Mtu aseme:

“´Abdur-Rahmaan, ´Abdullaah, ´Abdu-´Aziyz, ´Abdul-Kariym na mfano wa hayo.

Kafiri akisilimu, ikiwa jina lake si zuri linabadilishwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alibadili majina ya watu ambao wamesilimu na majina yao hayakuwa mazuri, hivyo akayabadili Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa majina mazuri. Ama jina likiwa halina maana mbaya, halibadilishwi. Jina halibadilishwi isipokuwa kama lina uabudiwa kwa asiyekuwa Allaah, kama mfano wa ´Abdul-Masiyh, ´Abdul-´Uzza, ´Abdul-Laat na mfano wa hayo. Jina likiwa na uabudiwa kwa asiyekuwa Allaah ni lazima kulibadili, ama ikiwa halina maana mbaya na halina uabudiwa kwa asiyekuwa Allaah, halibadilishwi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/1962
  • Imechapishwa: 06/10/2020