Swali: Ufaransa tunasoma kiarabu msikitini. Je, inajuzu kwa kafiri kuingia msikitini ili ajifunze lugha ya kiarabu?

Jibu: Ni sawa. Inafaa kwa kafiri akaingia msikitini. Manaswara waliingia msikitini kumtembelea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ajili ya haja. Akamfungamanisha Thumaamah bin Athaal msikitini kabla hajasilimu. Inafaa kwa kafiri kuingia msikitini kwa ajili ya haja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tahid-25-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017