Kafiri anayefanya maovu anakatazwa?


Swali: Nikimuona kafiri anafanya uovu nimkataze au hapana?

Jibu: Ukimuona kafiri anafanya uovu usimkataze. Hukumu za Kiislamu hazimgusi. Lakini unachotakiwa kufanya ni wewe kumlingania katika Uislamu na kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, asimamishe swalah, atoe zakaah, afunge Ramadhaan na ahiji Nyumba. Lakini akiwa katikati ya watu ambao wanakemea maovu haya, basi anatakiwa kukatazwa. Hakatazwi kwa sababu hukumu za Kiislamu zinamgusa. Bali anakatazwa kwa sababu ameenda kinyume na nidhamu za nchi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/851
  • Imechapishwa: 24/04/2018