Kafiri anaogopa kusilimu asije kuuawa baadae akiritadi


Swali: Kuna mtu kutoka Marekani anasema kuwa anasoma nje ya nchi na kusema ya kwamba pindi anapolingania katika dini ya Allaah anakabiliwa na utata kutoka kwa baadhi ya wale anaowalingania. Wanauliza kama watauawa endapo watasilimu kisha baadaye waritadi. Hili kwa kuzingatia ya kwamba kuna uhuru wa dini ndani ya nchi. Nimjibu vipi?

Jibu: Mwambie silimu, umuombe Allaah uthabiti na achana na wasiwasi. Achana na wasiwasi. Wewe umesilimu kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Silimu na uwe na nia nzuri. Muombe Allaah uimara katika dini na achana na wasiwasi huu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-13.mp3
  • Imechapishwa: 08/06/2018