Kafiri aliyesimulia katika Ramadhaan analazimika kutoa Zakaat-ul-Fitwr?

Swali: Zakaat-ul-Fitwr inawamujibikia mtu ambaye amesilimu katika Ramadhaan?

Jibu: Ndio. Analazimika kutoa Zakaat-ul-Fitwr kwa sababu ni muislamu. Katika Hadiyth ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefaradhisha Zakaat-ul-Fitwr pishi ya tende au pishi ya shayiri kwa mvulana na msichana, muungwana na mtumwa, mdogo na mkubwa katika waislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/259)
  • Imechapishwa: 21/06/2017