Kafara kwa anayekula kwa sababu ya kumuokoa mwengine

Swali: Yule ambaye anaacha kufunga kwa sababu ya kumwokoa mtu mwengine anaweza kulinganishwa na mjamzito pale anapoacha kufunga kwa kuchelea juu ya mtoto wake? Nakusudia atatakiwa kulipa na kulisha chakula?

Jibu: Inafaa kwa mtu kuacha kufunga kwa ajili ya kumuokoa mwengine kutoka katika maangamivu jambo likipelekea yeye kula akiwa hawezi kufanya hivo isipokuwa kwa kula. Katika hali hiyo inafaa kwake kula na kulipa.

Swali: Je, analazimika kutoa kafara pamoja na kulipa?

Jibu: Kuhusu kafara siwezi kukata kitu. Lakini kulipa analazimika kulipa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/410)
  • Imechapishwa: 22/03/2022