Swali: Ni ipi hukumu ya kununua kwa kadi ya mkopo ikiwa mtu analipa ndani ya muda na hivyo anaepuka ile ribaa?

Jibu: Kadi ya mkopo haijuzu kwa sababu inahusika na ribaa. Wanakulipia bili yako ambapo wanaongeza malipo yako. Hawakukupa nayo bure. Wanaongeza malipo yako kwa kila bili wanayokulipia. Hii ni ribaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 19/02/2022