Kaa na familia yako uwafunze na acha kuzurura na Jamaa´at-ut-Tabliygh


Swali: Kuna mtu anatoka na Jamaa´at-ut-Tabliyh na watoto wake hawaswali na anasema kuwa hana cha kuwafanya kwa sababu amewanasihi mara nyingi sana.

Jibu: Akae na watoto wake na apambane nao. Asitoke kwenda kuwafunza watu na akawaacha walioko chini ya mikono yake. Anatakiwa kuanza na wale walioko chini ya mikono yake. Awasimamie na amtake msaada Allaah kisha mamlaka husika. Mamlaka husika haikutengwa isipokuwa kwa kazi kama hizi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/حكم-من-يدعو-الناس-واولاده-لا-يصلون
  • Imechapishwa: 20/09/2022