Jukumu la wanafunzi


Swali: Katika mji wetu kumekithiri kuyaabudu makaburi. Baadhi ya walinganizi hawajali kuyakataza mambo kama haya. Unatunasihi nini sisi na wao juu ya suala kama hili?

Jibu: Kuwabainishia, kuwafunza na kuwaelekeza. Allaah atamwongoza amtakaye. Nanyi mtalipwa ujira.  Ama kuwanyamazia na kuwaacha, Allaah atakuulizeni siku ya Qiyaamah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ

“Haiwapasi waumini watoke wote pamoja kwenda [katika Jihaad]. Basi ni kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao kundi moja wajifunze dini na ili waonye watu wao watakaporudi kwao ili wapate kutahadhari.”[1]

Inawahusu wanafunzi. Hili ndilo jukumu lenu; kueneza dini, kueneza ulinganizi kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kuwafunza watu.

[1] 09:122

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (61) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid-%2029%20-0%206-1438.mp3
  • Imechapishwa: 06/08/2017