Swali: Wanafunzi wengi hii leo wamekuwa ni wenye kutilia umuhimu vitabu vya kifikra na vya kisiasa na wanapuuza kusoma vitabu vya Shaykh Muhammad  [bin ´Abdil-Wahhaab] na vitabu vya Salaf katika ´Aqiydah na mengineyo. Ni zipi nasaha zako juu ya hilo?

Jibu: Nasaha zetu ni kwamba walinganizi, waelekezaji na waalimu wasimame kuwaelekeza watu hawa, kuwabainishia njia sahihi na kubainisha mifumo inayoenda kinyume. Wakiachwa hapana shaka kwamba kila mmoja atafuata njia isiyokuwa sahihi. Ni lazima kuwepo walinganizi wanaolingania katika dini ya Allaah, waelekezaji na waongozaji, waalimu na watengenezaji. Ni lazima yapatikane haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqatu Da´wat-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17206
  • Imechapishwa: 01/01/2018