Swali: Umetaja katika Khutbah ya kwamba kupatwa kwa jua ni jambo limezidi siku hizi kwa sababu ya kuzidi kwa maasi. Je, maasi yanaathiri kwa kutikisika kwa mambo?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba maasi yanaathiri. Lakini taathira haiwi katika maasi kwa dhati yake. Bali maasi ni sababu. Ambaye anazibadilisha nyota ni Allaah (´Azza wa Jall). Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ

“Ufisadi umeenea katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyochuma mikono ya watu.” (40:41)

Kwa ajili hii ndio maana imekuja katika Hadiyth inayozungumzia kupatwa kwa jua:

“… ili aweze kuona ni nani atakayetubia upya.”

Allaah anakadiria hivo ili aweze kuona ni nani katika watu ambaye atatubia upya kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hayo yakafahamisha kwamba sababu ya kupatwa kwa jua ni maasi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/859
  • Imechapishwa: 27/06/2018