Josho kubwa linatosheleza wudhuu´

Swali: Nilioga josho la janaba kwa kutumia sabuni na shampoo. Je, josho hili linatosha kutohitajia kutia wudhuu´ ikiwa nitanuia jambo hilo?

Jibu: Linatosha hilo ukinuia twahara mbili. Bora ni yeye kutawadha kwanza kisha ndio aoge. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu ndio kamili zaidi. Hapana vibaya kutumia sabuni, shampoo, sidiri na vyenginevyo vinavyoondosha uchafu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/173)
  • Imechapishwa: 31/08/2021