Jiweke Mbali Na Hajaawirah


Swali: Muulizaji kutoka Uholanzi. Tunateswa na wafuasi wa al-Hajuuriy na khaswa wanawaingiza wanafunzi wapya nyuma ya mwanga. Unapendekeza kitabu ”al-Bayaan al-Fawriy” cha Shaykh ´Arafaat al-Muhammadiy ambacho Shaykh ´Ubayd amekiandikia utangulizi?
Jibu: Ndio, nakipendekeza. Ni kitabu kizuri.

Kadhalika ninawanasihi kujiweka mbali na al-Hajuuriyyuun. Jiwekeni mbali nao. Msijadiliani nao. Msiteti nao. Ni watu wa fujo na talbisi. Wanaingia ndani ya Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo Shaykh Muqbil mara nyingi alikuwa akipendekeza wanafunzi zake kuihifadhi Hadiyth wakati anaposafiri kwa ajili ya Da´wah, nayo ni Hadiyth ya Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna watu waliopotea baada ya kuwa wameongoka isipokuwa ni kwa ajili ya mjadala.”

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasoma:

مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا

Hawakukupigia [mfano huo wa kulinganisha] isipokuwa tu kutaka kujadili.” (43:58)

Imepokelewa na at-Tirmidhiy katika “al-Jaamiy´” kwa isnadi Swahiyh.

Walipotea baada ya uongofu waliokuwemo. Wakabadilika kutoka katika kulingania kwenye Sunnah na kulingania katika fitina, mijadala, fujo, magomvi na talbisi.

Jiweke mbali nao na tahadharisha kujiweka nao mbali. Ambao Allaah Amewawafikisha katika watu wa kheri watafuata Qur-aan na Sunnah na kupita katika njia ya wanachuoni ambao wanafuata Qur-aan na Sunnah. Jiweke mbali na njia ya Abul-Hasan al-Miswriy, njia ya al-Hajuuriy na wale wenye kupita katika njia yao katika wale ambao wameshikamana na taasisi (jumuiya) na makundi ya siasa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.darulhadith.com/v2/hall-dig-borta-fran-hadjuriyyah/
  • Imechapishwa: 18/01/2017