Swali: Ni upi wajibu wa muislamu pale ambapo fitina na vurugu inakuwa nyingi na baadhi wanaita katika kumfanyia mtawala uasi na wanaita kuwa ni “Jihaad”?

Jibu: Ni juu yako kuwa na uthabiti katika ´Aqiydah sahihi. Ni juu yako kujitenga mbali na walinganizi hawa; usisuhubiane nao na wala usichanganyike nao. Usiwasikilize wao, mikanda yao wala maneno yao. Wanaita katika kumuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kumuasi mtawala muumini ni kumuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule anayemtii kiongozi basi amenitii mimi na yule mwenye kumuasi kiongozi basi ameniasi mimi.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_27-07-1433.mp3
  • Imechapishwa: 23/05/2018