Swali: Niliolewa na mwanamume Suufiy ambaye alikuwa na mambo ya ushirikina. Lakini kwa uafikisho wa Allaah nikatalikiana naye na nilikuwa nimekwishazaa naye watoto. Hivi sasa nataka kuhajiri na mume wangu wa pili kwa sababu naishi katika nchi ya kikafiri. Ni zipi nasaha zako kwangu juu ya watoto?  Nimwachie nao yeye au nifanye kila niliwezalo ili niwachukue pamoja na kuzingatia ya kwamba na katika nchi hii ya kikafiri ya kikafiri ambayo tunaishi ndani yake hawawaruhusu watoto kusafiri isipokuwa kwa ruhusa ya baba yao. Naomba nasaha zako.

Jibu: Jitahidi uhajiri pamoja nao vovyote utavyoweza. Jitahidi usafiri nao. Usipoweza basi hajiri mwenyewe. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) waliacha mali zao na watoto wao Makkah na wakahahama pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hama japokuwa utakuwa huna watoto wako. Huko mbeleni muombe Allaah na ufanye sababu wakufuate. Wakiwa wakubwa watakuja na watamwacha baba yao ikiwa watakuwa wema. Ama wakiharibika basi kutakuwa hakuna kheri yoyote kwao na wala watakuwa hawana manufaa. Lakini wakiwa wema watakujia kwa idhini ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/02.mp3
  • Imechapishwa: 21/09/2018