Jirani kafiri ambaye haswali hatakiwi kusaidiwa


Swali: Nikiwa na jirani ambaye anaishi karibu na nyumba yangu haswali. Lakini hata hivyo nyumbani kwake kuna ambao wanaswali. Je, niache kuwaahidi kuwapa swadaqah na zawadi kwa ajili yake au niwanuie wale ambao wanaswali walioko nyumbani kwake? Ni ipi hukumu ya yule asiyeswali ikiwa nimeshamnasihi mara nyingi?

Jibu: Kuhusu kipande cha kwanza cha swali jibu tunamwambia ndio. Tangamana vizuri na jirani zako hata kama katika wao kutakuwa ambao hawaswali midhali wengi walioko nyumbani wanaswali. Ama ikiwa wote hawaswali – tunaomba ulinzi kwa Allaah – kama hali ilivyo katika baadhi ya familia, basi watu hawa hawastahiki kupewa swadaqah wala kutendewa wema. Kwa sababu watu hawa hawakubaliwi juu ya dini yao. Tofauti na jirani ambaye asili yake ni kafiri au kwa msemo mwingine haikutokea kwake kuritadi. Huyu mtendee wema. Kwa ajili hii wanachuoni wamesema kwamba kuna sampuli tatu za majirani:

Ya kwanza: Jirani ambaye ni muislamu na ni ndugu. Huyu ana haki ya Uislamu na haki ya udugu.

Ya pili: Jirani ambaye ni kafiri na ni ndugu. Huyu ana haki ya udugu na haki ya ujirani.

Ya tatu: Jirani ambaye si ndugu. Huyu ana haki ya ujirani.

Ama ikiwa ni ukafiri wa kuritadi – tunaomba ulinzi kwa Allaah – kama yule ambaye haswali, huyu hastahiki kusaidiwa kitu na wal asipewe swadaqah kwa chochote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/828
  • Imechapishwa: 25/03/2018