Jinsi ya mtoto kutangamana na wazazi wenye kugombana

Swali: Mama na baba wamegombana na mama yangu ananiamrisha kumuasi baba yangu. Ni ipi nasaha yako kwa hilo na ni wajibu kwangu kumtii?

Jibu: Hapana. Usimtii katika kumuasi baba yako na kumkasirikia baba yako. Watendee wote wawili wema. Mtendee wema mama yako na baba yako. Usimtii katika hili. Haya ni maasi na hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majid%20%207%20-%205%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 06/10/2020