Jinsi ya kuwasalimia kundi la watu waliokaa katika kikao


Swali: Je, ni katika Sunnah mtu akiingia kwa watu waliokaa kuwasalimia kwa kuwaashiria mkono pasina kupeana nao mkono?

Jibu: Ikiwa ametoka katika safari, apeane nao mikono. Ama ikiwa yuko katika mji na hakutoka safari inatosheleza kwake kuwatolea salamu. Hili linatosheleza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13221
  • Imechapishwa: 20/09/2020