Jinsi ya kutoa salamu baada ya swalah


Swali: Anapomaliza mwenye kuswali Swalah yake na akataka kutoa Salaam, je aseme “as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakatuh”, kuliani kisha kushotoni.” Au niseme “as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi”, tu? Na ni ipi hukumu ya mwenye kufanya hivyo kwa kuzidisha “… wa Barakatuh”?

Jibu: Lililothibiti katika Sunnah ni kusema “… wa Barakatuh” tu, hii ndio iko katika Shari´ah, kusema “as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaah” tu, hili ndilo liko katika Shari´ah. Nako ni kusema “as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi”, kuliani na kushotoni. Ama kuzidisha “… wa Barakatuh”, wanachuoni wametofautiana. Na kapokea ´Alqamah (Radhiya Allaahu ´anhu) kutoka kwa baba yake kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema namna hii: “as-Salaam ´alaykum wa Rahmatu-llaahi wa Barakatuh”. Lakini Riwaayah hii ya ´Alqamah ina tofauti. Kuna wanachuoni amb-ao wameisahihisha kutoka kwake, na kuna wanachuoni ambao wam-esema kuwa imekatika (isnadi yake). Muislamu anatakiwa asizidishe, aula na bora zaidi aishie kwa kusema “… wa Rahmatullaah.” Na mwenye kuzidisha kwa kudhani kuwa ni sahihi au hajui mambo haya, hakuna neno na Swalah yake ni sahihi. Lakini bora zaidi ni kutozidisha. Hivi ndivyo walivyosema wanachuoni. Na kufanyia kazi jambo lililothibiti na lenye nguvu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 30/03/2018