Swali: Jini ana taathira kwa mtu au mtu kumuathiri jini na kijicho kina taathira kwa yule mkusudiwa?

Jibu: Jini kumuathiri mtu na mtu kumuathiri jini na taathiri ya kijicho kwa yule mkusudiwa yote hayo ni mambo yanayotokea na ni yenye kujulikana. Lakini hata hivyo yote hayo yanakuwa kwa idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ya kilimwengu iliyokadiriwa na sio idhini Yake ya Kishari´ah.

Ama kuhusu taathira ya kijicho kwa yule anayemfanyia kijicho ni jambo limethibiti kimatendo na linatokea kwa watu. Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

”Kijicho (al-´Ayn) ni kweli. Lau kungelikuwa na kitu chenye kuitangulia Qadar basi kijicho kingeliitangulia.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakuna Ruqyah isipokuwa ni kutokamana na kijicho na homa.”

Hadiyth zenye kuhusiana na mada hii ni nyingi. Tunamuomba Allaah afya na thabati katika haki.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/174)
  • Imechapishwa: 24/08/2020