Jini linaweza kujibadili umbile la mtu au nyoka?

Swali: Je, Jini linaweza kujibadili umbile la mtu na la nyoka?

Jibu: Ndio linaweza. Kama anavyosema Allaah (´Azza wa Jall) katika Kitabu Chake:

إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لاَ تَرَوْنَهُمْ

“Hakika yeye na kabila yake wanakuoneni, na nyinyi hamuwaoni.” (al-A´raaf 07:27)

Anaweza kuja kwa sura ya paka, mbwa na mbwa nyeusi ni Shaytwaan au sura ya nyoka na kinyume na hivyo kama ilivyotokea wakati Swahabah mmoja alichukua mkuki na akaipiga nayo ikamshambulia, na haijulikani nani kati yao alieanza kufa mwanzo. Kisha akasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika Madiynah kuna kundi la majini, basi mtapoona viumbe [mfano wa nyoka] katika manyuma yao, aipe onyo kutoka mara tatu.”

Wanaweza pia kujibadili kwa rangi tofauti. Bali huenda hata mtu asiweze kuyaona kwa sura (umbile) lao na uhakika wao. Niliambiwa na mtu wa Sa´ada. Alikuwa anasoma Qur-aan na mwengine. Ilikuwa ni Jini lakiume likawa lamshindilia na kumuomba limuone kwa sura yake. Akaliambia kuwa hili haliko katika utashi wako wala utashi wangu. Likaendelea kumshindilia. Kama kwamba lilikuwa likimuonesha sura yenye kukera. Hivyo Jini likawa mtu. Kwahiyo huenda hayawezi kuonekana kwa sura yao aliyowaumbia kwayo Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/UtI4EqAkT4k
  • Imechapishwa: 10/04/2022