Jini la mahaba limemwandama


Swali: Ni ipi dawa kwa mwanamke ambaye amesibiwa na jini na linasema kuwa linampenda mwanamke huyu na ni mke wake pamoja na kujua kuwa hali hii imeendelea kwa miaka miwili sasa?

Jibu: Mwanamke huyu atibiwe kwa Ruqyah ya Kishari´ah. Asomewe Ruqyah ya Kishari´ah kwa wanachuoni waaminifu na watu wenye ujuzi wa Ruqyah ya kishari´ah. Wamsomee Ruqyah kwa kukariri – Allaah akitaka – ataponya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14725
  • Imechapishwa: 02/05/2018