Jimaa katika funga ya siku sita za Shawwaal

Swali: Kuna mtu amemjamii mke wake katika moja ya michana ya zile siku sita za Shawwaal. Je, kuna dhambi yoyote juu yake?

Jibu: Hana dhambi yoyote. Kafara ni kitu maalum katika mchana wa Ramadhaan. Hata kama inahusiana na deni la kulipa Ramadhaan. Endapo mke atalipa deni la Ramadhaan ambapo akamfanyia jimaa basi anapata dhambi lakini hata hivyo halazimiki kutoa kafara. Mtu ambaye analipa deni la Ramadhaan haifai kufungua; ni mamoja kwa jimaa au kwa kula. Funga yake ikiharibika pasi na udhuru basi anapata dhambi. Hata hivyo halazimiki kutoa kafara. Swawm ya zile siku sita za Shawwaal zimependekezwa. Ni jambo lina hukumu moja. Hakuna kitu juu yake wala dhambi. Akitaka kuilipa siku hiyo ni vyema. Asipoilipa basi hakuna neno kwa sababu ni swawm iliyopendekezwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 20/11/2020