Swali: Kuna mtu amefanya jimaa mchana wa Ramadhaan, akatoa kafara, halafu mchana huohuo akafanya jimaa tena. Je, atoe kafara kwa mara nyingine?

Jibu: Haya tumeyasoma punde tu. Mnasahau haraka. Akifanya jimaa kabla ya kutoa kafara kwa siku hiyohiyo moja, basi itamlazimu kafara moja. Na akifanya jimaa, kisha akatoa kafara, kisha akafanya jimaa, basi atalazimika kutoa kafara nyingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (18) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtfq-15011435-01.mp3
  • Imechapishwa: 28/11/2019