Jimaa baada ya mwanamke kutoka kwenye hedhi

Swali: Mume anaruhusiwa kumwingilia mke wake mwenye hedhi ambaye ametwaharika kabla ya kuoga?

Jibu: Hapana. Kitendo hichi kinaenda kinyume na Aayah:

وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ

“Wala msiwakaribie [ili kujimai nao] mpaka watwaharike kwanza. Watakapotwaharika basi waendeeni kupitia pale alipokuamrisheni Allaah.”[1]

Amefanya kumwingilia baada ya kupatikana mambo mawili:

1- Damu yake ikatike.

2- Aoge.

[1] 02:222

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (7) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–15041434.mp3
  • Imechapishwa: 18/03/2017