Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuvaa ´Abaa´ah ya mapambo, anaweka ´Abaa´ah mabegani na kuvaa suruwali?

Jibu: Suruwali haijuzu kwa mwanamke. Suruwali sio vazi la mwanamke. Mwanamke anatakiwa kuvaa vazi pana, lenye kusitiri na lililo la wasaa. Haijuzu kwake kuvaa mavazi ya kubana. Suruwali ni vazi la kubana. Haijuzu kwake.

´Abaa´ah la mapambo halijuzu. ´Abaa´ah ni kwa ajili ya kujisitiri. Sio kwa ajili ya kujipamba. ´Abaa´ah halitakiwi kuwa na mapambo na michoro.

Wakati anapotoka ´Abaa´ah anatatakiwa kuliweka juu ya kichwa. Hata hivyo hakuna neno akaliweka mabegani mwake anapokuwa nyumbani au pamoja na wanawake wenzake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’-ul-Jumu´ah bit-Twaa’if http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17101
  • Imechapishwa: 24/09/2017