Takriban mwaka mmoja uliopita kumejitokeza ´Iraaq na Shaam kipote kinachoitwa ISIS. Wanadai kuwa ni dola ya Kiislamu ilihali ni muendelezo wa Khawaarij ambao walizuka wakati wa Masahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), wakawakufurisha na wakawaua makhaliyfah waongofu ´Uthmaan na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa). ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) aliwapiga vita na akawaua. Jarima zao zimewafanya baadhi ya vijana na wapumbavu kuwaua watu wasiokuwa na hatia walipokuwa wamesimama na kuswali. Kitendo cha mwisho ni yale yaliyotokea kwenye msikiti wa SEF Asir pindi watu walipokuwa wamesimama na kuswali. Misahafu ilizama kwenye damu za waswalaji. Watu hawa wanadai kuwa matendo yao ni Jihaad na kufa shahidi. Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba ni Jihaad katika njia ya shaytwaan.

Ni kwa akili na dini ipi ni Jihaad na kufa shahidi kuwaua waswalaji na kuizamisha misahafu kwa damu zao? Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba kuiua nafsi pasi na haki ni dhambi bila ya kujani yatapitika wapi. Mtu asemeje kitendo kama hicho kikipitika wakati wa swalah msikitini? Ni dhambi kubwa. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَٰلِكَ فِي الْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ

“Kwa ajili ya hivyo, Tukawaandikia wana wa Israaiyl kwamba; atakayeiua nafsi bila ya yeye mwenyewe kuua au kufanya ufisadi katika ardhi, basi ni kama ameua watu wote. Na atakayeiokoa basi ni kama amewaokoa watu wote. Na bila shaka walifikiwa na Mitume Wetu kwa hoja bayana, kisha wengi miongoni mwao baada ya hayo wamekuwa wapindukao mipaka ya kuasi. (05:32)

Madhambi haya yakupindukia yanaenda kinyume na ule wasifu ambao Allaah (Ta´ala) amemsifu kwao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ

“Basi ni kwa Rahmah kutoka kwa Allaah umekuwa mpole kwao. Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu wangelitawanyika mbali nawe.” (03:159)

Vilevile unaenda kinyume na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika Allaah ameandika wema juu ya kila kitu. Hivyo pale mnapoua, ueni vizuri. Pale mnapochinja, basi chinjeni vizuri. Noeni vizuri visu vyenu na mwache mnyama wenu astarehe.” (Muslim)

Allaah ameharamisha kwa mtu ambaye anaiua nafsi pasi na haki kuwa ni mwenye kuahidiwa kuwa shahidi na Pepo! Mtu kama huyu ameahidiwa Moto. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا

“Na atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni [Moto wa] Jahannam, ni mwenye kudumu humo na Allaah Atamghadhibikia na Atamlaani na Atamuandalia adhabu kuu.” (04:93)

Ni vipi itawezekana Shari´ah yenye kufikishwa na mtu ambaye Allaah amemsifu ifuatavyo:

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ

“Na Hatukukutuma isipokuwa uwe ni Rahmah kwa walimwengu. (21:107)

ataruhusu kuwaua watu bila ya haki ambao wanaswali misikitini na misahafu ikazama kwenye damu zao? Tunajilinda kwa Allaah kutokamana na hali za upindaji:

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ

“Ee Mola wetu! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoza na Tutunukie kutoka kwako Rahma. – Hakika Wewe ni Mwingi wa kutunuku na kuneemesha.” (03:08)

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://al-abbaad.com/index.php/articles/139-136
  • Imechapishwa: 06/11/2016