Jihaad inategemea na uwezo wa waislamu

Swali: Leo wakati waumini wamekuwa madhaifu, kuna baadhi yao wanasema “Hatuna nusura isipokuwa tutapopigana Jihaad katika njia ya Allaah na udhalili uliotupata ni kwa sababu ya kuacha kupigana Jihaad katika njia ya Allaah”. Je, kauli hii ni sahihi?

Jibu: Kupigana Jihaad katika njia ya Allaah ni wajibu wakati wa uwezo. Ama ikiwa hatuna uwezo wa kupigana Jihaad, Jihaad inakuwa haikuwekwa kwetu kwa kuwa hili litakuwa na madhara kwa Waislamu:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake.” (02:286)

Jihaad inakuwa wakati wa uwezo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipokuwa Makkah hakuwa anapigana Jihaad. Alikatazwa Jihaad. Kwa kuwa Waislamu hawakuwa na uwezo. Lau angelipigana Makkah kungelipatikana madhara. Pindi alipohamia al-Madiynah na akawa na nguvu pamoja na Answaar na wasaidizi, hapo ndipo Allaah Aliweka Jihaad. Jihaad inategemea na uwezo wa Waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (64) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13821
  • Imechapishwa: 16/11/2014