Jihaad bora katika vyombo vya mawasiliano

Swali: Je, Hadiyth inayosema “Jihaad bora ni neno la haki mbele ya mtawala dhalimu” inaweza kutumiwa juu ya ambaye anamkemea mtawala kwenye vyombo vya mawasiliano?

Jibu: Hapana. Hadiyth inasema “mbele ya mtawala”. Hiyo maana yake ni kwa mdomo mbele yake. Hakusema amkemee juu ya mimbari na kwenye barabara. Ameseme “mbele yake”. Allaah (Jalla wa ´Alaa) alisema kumwambia Muusa na Haaruun:

اذْهَبَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ

“Nendeni kwa Fir’awn – hakika yeye amevuka mipaka ya kuasi – mwambieni maneno laini, pengine akawaidhika au akakhofu.”[1]

[1] 20:43-44

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls–1434011.mp3
  • Imechapishwa: 30/07/2021