Jifunze dini yako na achana Jamaa´at-ut-Tabliygh!

Swali: Maswali yamekuwa mengi kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh.

Jibu: Jamaa´at-ut-Tabliygh wanajulikana vyema kuwa ni Suufiyyah. Hatumshauri yeyote kutoka nao. Kwa kuwa hawalinganii katika Tawhiyd, hawaamrishi mema na wala hawakatazi maovu. Wanawaamrisha watu kufanya Khuruuj kwa siku 40, miezi 3, mara 2 kwa kila wiki na kwa mwezi mara 3. Yote haya hayana dalili. Hizi Khuruuj wanaita kuwa ni ´katika njia ya Allaah` na wanachotilia umuhimu ni Adhkaar peke yake. Wanaofanya hivi ni ´Awwaaam wasiokuwa na elimu.

Tunawanasihi vijana kulazimiana na duruus na kutafuta elimu. Wasitoke. Baada ya hapo mtu akitaka kulingania afanye hivo. Ama kutoka hali ya kuwa ni mjinga asiyejielewa, hafahamu lolote, si sawa. Wanawapitisha mbele baadhi ya wazee wakubwa wasiojua lolote na hawakusoma! Mtu ambaye hajui kusoma wala kuandika wanampitisha mbele Msikitini aongee na atoe nasaha! Kadhalika wanawapitisha mbele vijana ambao hawakusoma! Mtu anapozungumza masuala ya Tawhiyd hawamuachi. Bali kinyume chake wanamkataza na kumwambia usilinganie katika Tawhiyd, usiamrishe mema na wala usikataze maovu. Zungumzia mambo mengine na wala usimzungumzie yeyote.

Makusudio ni kwamba tunawanasihi vijana kulazimiana na kutafuta elimu, kujifunza na kuwa na uelewa katika Dini. Halafu baada ya hapo mtu anaweza akawalingania watu katika Dini ya Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4743
  • Imechapishwa: 01/05/2015