Jiepushe na vitabu vya al-Kawthariy na Abu Ghuddah

Swali: Nilikuwa napenda kujua mtu huyu ´Abdul-Fattaah Abu Ghuddah aliyefariki. Nimepewa kitabu kilichoandikwa na yeye kinachoitwa “Qiymat-uz-Zaman ´indal-´Ulamaa”.

Jibu: Abu Ghuddah huyu pointi nyingi dhidi yake. Kiongozi na Shaykh wake ni al-Kawthariy. al-Kawthariy amemkufurisha Ibn Taymiyyah na mfano wake na kusema kuwa walikuwa wapotevu. Abu Ghuddah anamnusuru na anajifakharisha naye. Sijui ni hali ipi alokufa juu yake. Hata hivyo vitabu vyake havitakiwi kusomwa. Sipendelei visomwe. Katika vitabu vya wanachuoni wa Salafiyyuun kuna yenye kutosheleza, sawa ikiwa ni kuhusiana na Hadiyth au elimu nyingine yenye kunufaisha. Muulizaji anatakiwa kujiepusha na vitabu vya Abu Ghuddah, al-Kawthariy na mfano wao ambao wametumbukia katika Bid´ah zinazopingana na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=143736
  • Imechapishwa: 11/03/2017