Jiepushe kuwasikiliza wazushi kama al-Qarniy, Khaalid ar-Raashid na Nabiyl al-´Awadhwiy


Swali: Je, inajuzu kusikiliza mihadhara ya ´Aaidh al-Qarniy, Nabiyl al-´Awadhwiy na Khaalid ar-Raashid…

Jibu: Tunakunasihi kutosikiliza mihadhara ya wazushi na watu wa Bid´ah na matamanio. Jiepushe nao. Usipoteze wakati wako pamoja nao. Batili ndio inapitika katika ndimi zao watu wa Bid´ah, watu wenye kufuata matamanio na wengineo. Batili ndio inapitika katika ndimi zao [… sauti haiko wazi…]. Si watu waliofungamana na Qur-aan na Sunnah. Lau wangelifungamana na Qur-aan na Sunnah katika maneno na matendo yao wasingelikuwa watu wa Bid´ah. Lakini pindi walipokuwa si watu waliofungamana na Qur-aan na Sunnah ndipo batili ikawa ni yenye kupitika kwenye ndimi zao. Huenda wakaisema kwa njia ya dini na huku wakiona kuwa ni haki kwa mtazamo wao. Nakunasihi kujiweka mbali na wao na kutosheka na mihadhara ya wanachuoni waliobobea katika elimu na ambao ni wapole kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Katika darsa zao, mihadhara yao na Khutbah zao kuna kheri nyingi na yenye kutosheleza.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=wF9OYBaYvjE
  • Imechapishwa: 28/01/2018