Je, wazazi wawili wanalipwa thawabu kwa kila kitendo wanachofanya watoto?

Swali: Je, wazazi wawili wanalipwa thawabu kwa kila kitendo wanachofanya watoto ikiwa watajitahidi kuwalea mpaka wape watapofikisha ile miaka ya baleghe?

Jibu: Ndio, Allaah akitaka. Abu Hurayrah ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote anayelingania katika uongofu basi anapata ujira mfano wa yule mwenye kumfuata pasi na kupungua chochote katika ujira wao.”

Tusemeje kwa ambaye amewalea watoto? Kuwalea watoto na kuwafunza mambo ya kheri ni jambo lina fadhilah kubwa zaidi.

Swali: Jukumu la wazazi wawili linamalizika kwa watoto kufikisha ile miaka ya baleghe? Nakusudia upande wa Shari´ah pindi wanapofanya makosa au madhambi wazazi wawili nao wanapa dhambi?

Jibu: Hapana:

وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ

“Wala habebi mbebaji mzigo [wa dhambi] wa mtu mwengine.” (06:164)

Ni lazima kuwanasihi, kuwaelekeza mambo ya kheri, kuwakataza maovu, kuwahimiza kuwa na msimamo, kuacha mambo maovu na kadhalika.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-07-03-1438-هـ
  • Imechapishwa: 20/06/2022