Swali: Je, wafu huzijua hali za waliohai?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kimsingi ni kwamba hawajui. Kwa sababu maiti matendo yake yote yameshakatika:

إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ

“Hakika wewe huwezi kusikilizisha wafu.” (27:80)

Huu ndio msingi ya kwamba hawajui. Lakini kumepokelewa kitu kinachofahamisha kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapotolewa salamu basi Allaah humrudishia roho yake na akamwitikia salamu yule mtoaji. Kilichowekwa katika Shari´ah kwa yule muislamu ni yeye kuwatolea salamu wale wafu. Hili ni jambo maalum. Sisi hatujui hali zao. Hata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imepokelewa katika Hadiyth mbalimbali ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Naonyeshwa matendo ya Ummah wangu – mema na maovu – akafurahi kwa yale mema na akaomba msamaha kwa yale maovu.”

Lakini Hadiyth hii ni dhaifu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/19/%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%82%D8%A7%D8%A1-%D8%A3%D8%B1%D9%88%D8%A7%D8%AD-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%88%D8%AA%D9%89%D8%8C-%D9%88%D8%B9%D9%84%D9%85%D9%87%D9%85-%D8%A8%D8%A3%D8%AD%D9%88%D8%A7%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%A3%D8%AD%D9%8A%D8%A7%D8%A1
  • Imechapishwa: 30/11/2019