Je, uwajibu wa swalah ya ijumaa unaanguka ikiwa ´Iyd itaangukia siku ya ijumaa?

Swali: Je, uwajibu wa swalah ya ijumaa unaanguka ikiwa ´Iyd itaangukia siku ya ijumaa?

Jibu: Ndio. Kuna Hadiyth juu ya hilo:

“Hakika katika siku yenu hii zimekutana sikukuu mbili. Yule anayetaka hahitajii kuswali swalah ya ijumaa. Kwa hali yoyote tutaswali swalah ya ijumaa.”[1]

Kuna udhaifu ndani yake.

Imethibiti vilevile kwamba pindi ´Abdullaah bin az-Zubayr alipokuwa gavana wa Makkah watu walimsubiri atoke ili waswali, lakini hata hivyo hakutoka. Wakati walipomuuliza Ibn ´Abbaas juu ya hilo akasema:

“Ameiafiki Sunnah.”

Lakini hata hivyo bado ni wajibu kuswali Dhuhr. Yule ambaye hakuswali swalah ya ijumaa ni wajibu aswali Dhuhr.

[1] Imaam al-Albaaniy amesema:

”Swahiyh.” (Swahiyh Sunan Ibn Maajah (1/392))

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=847
  • Imechapishwa: 14/06/2018