Je, thawabu za hajj zinapungua mtu akisafiri kwa gharamu za mtu mwingine?

Swali: Mwanamke huyu anasema kwamba amedangana sana. Ametekeleza faradhi ya hajj – na himdi zote anastahiki Allaah – lakini kinachonifanya kudangana na kuwa na wasiwasi juu ya upungufu wa hajj yangu ni kwamba mimi sikugharamikia zile thamani zake. Aliyegharamikia hayo ni mmoja katika wahisani kwa sababu mshahara wa mume wangu ulikuwa mdogo. Mimi wakati huo nilikuwa namiliki dhahabu kidogo. Nachelea hajj yangu isije kuwa yenye mapungufu kwa sababu sikuuza dhahabu hii ili nigharamikie gharama hizo.

Jibu: Hajj sio pungufu – Allaah akitaka. Nataraji kwa Allaah kwamba ni yenye kukubaliwa. Wala sio lazima kuuza dhahabu yake ili aweze kuhiji. Kwa sababu dhahabu ni miongoni mwa mahitajio ya kimaumbile ambayo ni lazima mwanamke awe nayo. Kwa hiyo sio lazima aiuze ili aweze kuhiji. Hivyo namwambia mwanamke huyu: tulia! Hajj yako ni sahihi na umetekeleza dhimma yako. Umeshatekeleza faradhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/981
  • Imechapishwa: 28/12/2018