Je, swalah inasihi kwa Tasliym moja?


Swali: Je, swalah inasihi kwa Tasliym moja?

Jibu: Mtu anapaswa kutoa Tasliym mbili. Hii ndio Sunnah. Kuhusu Tasliym ya kwanza ni wajibu na Tasliym ya pili wanachuoni wametofautiana. Wanachuoni wengi wanaona kuwa ni wajibu kuleta Tasliym zote mbili. Baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa Tasliym ya pili ni Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 14/10/2018