Je, sungura ni halali kumla?


Swali: Ni ipi hukumu ya kula sungura kwa kuwa wapo watu wamesema kuwa anapata hedhi na hivyo haijuzu kumla?

Jibu: Sungura ni halali hata kama atapata hedhi. Imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimla na Maswahabah wakamla. Kwa hivyo hakuna neno kumla. Sungura ni halali kabisa japokuwa atapata hedhi. Kuna wanachuoni waliosema kuwa anapata hedhi. Hata kama anapata hedhi hilo halidhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.binbaz.org.sa/noor/3147
  • Imechapishwa: 24/03/2018