Je, ni sahihi kuoga kwa maji na sabuni mchana wa Ramadhaan?

Swali: Je, ni sahihi kuoga kwa maji na sabuni mchana wa Ramadhaan? Je, kuota kunamfunguza mwenye kufunga? Je, manukato yanafunguza?

Jibu: Mosi: Inajuzu kwa mfungaji kuoga kwa maji na sabuni mchana wa Ramadhaan.

Pili: Mwenye kuota mchana wa Ramadhaan ilihali amefunga swawm yake haiharibiki. Ni juu yake kuoga ikiwa ametokwa na manii.

Tatu: Mwenye kujitia aina yoyote ya manukato mchana wa Ramadhaan swawm yake haiharibiki. Lakini hata hivyo asitumie zile aina za manukato ya kufukiza kama ufukizo wa miski.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/272)
  • Imechapishwa: 11/06/2017