Je, ni lazima kwa mwanamke kuosha ndani ya uke pindi anapooga janaba au hedhi?

Swali: Mmoja mmoja ameambiwa kwamba endapo atakuwa na janaba basi asitawadhe isipokuwa baada ya kuingiza maji ndani ya uke. Je, hayo ni sahihi?

Jibu: Sio wajibu kwa mwanamke pindi anapooga janaba au hedhi kuosha ndani ya uke. Haya ndio maoni sahihi zaidi katika maoni mawili. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/296-297)
  • Imechapishwa: 14/11/2017