Je, ni kweli al-Fawzaan kawasifia Jamaa´at-ut-Tabliygh?

Swali: Je unaninasihi kutoka na Jamaa´at-ut-Tabliygh khaswa tunavyosikia kuwa umesifia kikundi hiki siku zilizopita?

Jibu: Mwenye kusema kuwa mimi nimewasifia ni muongo. Mimi sikuwasifia. Mimi sisifii isipokuwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao wanalingania katika Tawhiyd, katika ´Aqiydah sahihi, wanawafunza watu elimu yenye manufaa. Watu hawa ndo ambao tunawanasihi Waislamu kuwa pamoja nao. Ama watu wa Bid´ah na watu wasiofahamu Tawhiyd na wala hawaiwekei uzito na wanafanya Bid´ah, watu hawa tunatahadharisha watu dhidi yao vikali.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=128423
  • Imechapishwa: 03/09/2020