Je, ni dhuluma kumtaliki mwanamke bila sababu?

Swali: Vijana wengi wanawataliki wake zao na baada ya kumuoa kwa kipindi kifupi wanasema kuwa hawawapendi au sipendi rangi yake. Je, kufanya hivo ni katika dhuluma ikiwa hakuna sababu ya kukinaisha?

Jibu: Ni haramu kwake kusengenya. Huko ni kusengenya. Anatakiwa kumuombea sitara na afya. Lakini akimtaka ushauri mtu ambaye anataka kumuoa, basi anatakiwa kumshauri kwa anayoyajua. Kwa sababu hiyo ni nasaha.

Swali: Anaishi naye mwezi mmoja, miwili, mitatu au mwaka mmoja kisha anasema kuwa hampendi na kwamba anataka kumtaliki. Je, anakuwa mwenye kudhulumu kwa kule kumtaliki?

Jibu: Hili linarejea katika ile hali yake. Akiona manufaa ni kule kumwacha basi atafanya hivo. Hili limefungamana na manufaa.

Swali: Lakini mwanamke huyo anampenda?

Jibu: Haijalishi kitu. Ikiwa katika kubaki naye kuna manufaa atambakiza. Na akiona manufaa kwake ni kule kumtaliki basi atamtaliki. Yeye ndiye anaijua nafsi yake zaidi na yeye ndiye anaijua hali yake pamoja naye.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21551/هل-من-الظلم-الطلاق-دون-سبب-مقنع
  • Imechapishwa: 21/08/2022